Wakulima wa Korosho wasitisha mgomo

TANI 20,000 za Korosho ghafi zinatarajiwa kupelekwa kwenye minada ya pili msimu wa mauzo 2022/2023 ambayo inaanza leo sehemu mbalimbali ya mikoa ambayo inalima zao hilo

Kaimu Mkurungezi wa wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT) Alfred Francis amesema minada hiyo ya pili itaanza leo na kumalizika Novemba 3, mwaka huu.

Korosho tani 15, 000 kupelekwa mnadani

Francis, amesema Korosho hizo ni pamoja na Korosho tani 15,000 ambazo hazikuuzwa kwenye minada ya kwanza iliyoanza Oktoba 22 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi walikataa kuuza Korosho hizo tani 15,000 kwa madai kuwa bei iliyotangazwa na wanunuzi ni ndogo kuliko uzalishaji.

Katika Minada hiyo ambayo ilifanywa na vyama vya vikuu vya ushirika vya TANECU, MAMCU, RUNALI na Lindi Mwambao, bei ya juu ya korosho kwa kilo ilikuwa 2,200 na bei ya chini 1,480.

Lakii wakulima wakulima walisema bei hiyo haina maslahi na hivyo kukataa kuuza korosho ambazo zilirudishwa kwenye maghala zikisubiria Minada ya pili leo.

Habari Zifananazo

Back to top button