Wakulima wa pamba macho yote Shinyanga!
KISHAPU, Shinyanga: MACHO na masikio ya wakulima wa pamba nchini leo yapo mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kishapu, ambapo kunafanyika uzinduzi wa ununuzi wa zao hilo msimu wa 2023/24 utakaombatana na kutangazwa kwa bei.
Kupitia Bodi ya Pamba, serikali itatangaza rasmi bei ya kununulia zao hilo, ambapo kiu kubwa ya wakulima ni kuona au kusikia serikali inaongeza bei ya zao hilo tofauti na msimu uliopita mwaka jana.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/marufuku-wanunuzi-pamba-kuanzisha-vutio-binafsi/
Katika msimu wa ununuzi wa zao hilo uliopita 2022/23 ambao ulizinduliwa katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, serikali ilitangaza bei ya kuanzia kununulia zao hilo kwa kilo moja Sh.1,060.
Wakulima wengi walilalamikia bei hiyo, wakidai kuwa ni ndogo na haiwezi kuwaondoa katika wimbi la umaskini huku serikali ikieleza kuwa bei hiyo ilipangwa kwa kufuata bei elekezi ya soko la zao hilo.
Hata hivyo wakulima wakiwa na matumaini kuwa bei itapanda, wengi waliomba serikali kuangalia mfumo wa upangaji bei katika msimu wa mwaka huu ili iweze kuongezeka na wao waweze kunufaika zaidi.
Endelea kufuatilia ukurasa zetu kujua bei itakayotangazwa na serikali Leo hii.