Wakulima waonywa kununua mbegu nchi jirani

WAKULIMA wa zao la mahindi na mazao mengine ya chakula Wilaya ya Momba mkoani Songwe, wametakiwa kuacha kukimbilia kununua mbegu za mahindi nchi jirani ya Zambia, badala yake wajikite kununua mbegu bora zilizofanyiwa tafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Hayo yamezungumzwa na mtafiti wa zao la mahindi kutoka TARI Mbeya, Julias Sanga wakati wa ziara ya watalaam kutoka Wizara ya Kilimo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe kutoa elimu kuhusu kilimo chenye tija.

Amesema taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania ina mbegu nzuri hasa za mahindi, ambazo zinafanyiwa utafiti kulingana na ardhi ya maeneo husika ya Tanzania.

” Wakulima muache kukimbilia kununua mbegu Zambia kama alivyoeleza Mbunge wetu, kuwa wengi wenu mnatumia mbegu za nchi jirani ya Zambia, Tanzania tuna mbegu nzuri ambazo ni za uhakika , ambapo ukizingatia kanuni bora za kilimo unapata gunia 25 mpaka 30,” amesema Sanga.

Amesema kununua mbegu kutoka nchi nhyine ni kosa kisheria, Lakini pia inapunguza uzalishaji kwa sababu mbegu za Tanzania zinafanyiwa utafiti kulingana na mazingira husika.

Mbunge wa Jimbo la Momba Condester Sichalwe, alisema  wakulima wengi wamekuwa wakikosa mbolea, hivyo kujikuta wanapata mazao kidogo kutokana na wasambazaji wengi wa mbolea kuiuza mbolea nchini Zambia.

Alisema pia kutokana na changamoto ya miundombinu ya kutofikika kirahisi pamoja na kuuziwa mbegu feki katika jimbo lake , wakulima wengi wamekuwa wakikimbilia Zambia kununua mbegu za mazao hasa mahindi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Margaretarth
Margaretarth
2 months ago

I am now making more than 350https://s.w.org/images/core/emoji/14.0.0/svg/1f4b0.svg dollars per day by working online from home without investing any money.Join this link posting job now and start earning without investing or selling anything……. 
🙂 AND GOOD LUCK.:)..____ http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by Margaretarth
EmmyKeira
EmmyKeira
2 months ago

★I get paid more than $300 to $400 per hour for working online. ( o74w) I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily $20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
Here is I started.…………>> http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x