Wakulima wapata Sh bilioni 32 mauzo mbaazi
WAKULIMA wa zao la mbaazi ghafi mkoani Lindi wamepata Sh bilioni 32.8 msimu huu.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Terack amesema hayo leo Septemba 18, 2023 wakati akitoa taarifa ya mkoa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara sanjari kuweka Jiwe la Msingi katika barabara itokayo Nanganga Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara hadi Ruangwa Lindi.
Alisema miaka ya nyuma wakulima wa zao hilo walikuwa wanauza mbaazi ghafi kwa Sh 2000 kwa kilo moja.
Alifafanua baada ya kukubaliana na Wizara ya Kilimo kwa kuridhia kuuzwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kilo moja iliangukia Sh 2000 hadi Sh 2005.
RC huyo alieleza kuwa zao la ufuta iliweza wakulima kupata Sh bilioni 98 msimu huu. Aliongeza zao la korosho limeweza kuuza Sh bilioni 106 msimu uliopita.
Aidha mkoa ilikiwekea mkakati kuweza kuzalisha zaidi mazao hayo. Aliongeza ile tabia kuwa zao la mbaazi ni mboga sasa ni biashara.