Wakulima watumia mbegu za kisasa

ZAIDI ya wakulima 300 wanatumia mbegu za bora na za kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kupata faida zaidi kupitia sekta ya kilimo nchini.

Wakulima hao wamepata mbegu bora za alizeti, kupitia Mradi wa Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT) ambapo kampuni ya Highland Seeds Growers LTD iliyopo jijini Mbeya imekuwa ikiwapatia elimu na mbegu bora.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya waliofanya ziara katika wakati Kampuni hiyo Kaimu Meneja ,Elizabeth Mallya amesema ili kutekeleza mradi wa AMDT kupitia TARI Ilonga iliyopo Kilosa ,Morogoro wanashirikiana kutoa mbegu za msingi kwaajili ya kuzalisha wa mbegu za alizeti.

“Kwahiyo kutokana na ushirikiano huu tukaingia kuzalisha mbegu za alizeti na watafiti tunasaidiana nao kuchukua mbegu za msingi na kutusaidia shambani kwa kutoa maelekezo kama kuna tataizo tunawasiliana nao wanatupa huduma ,”ameeleza.

Amebainisha kuwa Katika kutekeleza mradi huo walipewa fungu na kuanza mwaka 2022 ambapo walifanikiwa kuzalisha tani 21 kupitia mradi wa AMDT kwa kulima nwa wakulima watatu kwa kuanza na kituo cha na tuliuza katika kituo cha Agriculture Seed Agency(ASA) .

Mallya amefafanua kuwa kwa kipindi cha mwaka huu walisaini mkataba wa kuzalisha mbegu za alizeti na wanategemea kuzalisha tani 100 ambapo tani 50 ziko katika usimamizi wa mradi wa AMDT na nyingine 50 inatokana na chanzo chao cha mapato cha mwaka 2022.

“Tumeingia kwenye mkataba na wakulima watatu na mmoja yuko Mbarali ,wawili wako Songwe wote wako katika hatua za uvunaji na tumelima ekari 140 tunategemea kupata tani 50 au zaidi,”amefafanua.

Aidha amesema wamekuwa wakifanya masuala ya masoko ambapo wakulima zaidi ya 200 walijifunza kilimo bora cha alizeti na kanuni bora za kilimo na maswali yao yalijibiwa ambapo pia wapo wakulima walinunua mbegu na kupitia mradi huu wanategemea kipindi cha msimu wa sikukuu ya wakulima nane nane kufikia wengi zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button