Wakulima wavuna gunia 400 za alizeti

JUMLA ya magunia 400 sawa na tani 25 ya alizeti yamevunwa kwenye shamba la ekari 70 ikiwa ni hatua ya mradi wa matumizi ya mbegu bora kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Mradi huo unaodhaminiwa na Taasisi ya Kuboresha Mifumo ya Masoko ya Kilimo nchini (AMDT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI).

Advertisement

Katika mradi huo zaidi ya wakulima 250 katika Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wameendelea kunufaika na kilimo cha mbegu bora za alizeti unaoratibiwa na serikali pamoja na wadau wa kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea shamba lililoko kijiji cha Kapumpa, Afisa wa Kilimo kutoka Lima Africa Company Limited, Roance Rwegasila amesema mradi umefanikiwa kutoka elimu, ajira na pembejeo kwa wakulima hao.

Kati ya wakulima hao wanawake ni 150 ni na vijana ni 100.

Amesema serikali inazalisha mbegu za awali aina ya Record na wao wanazalisha kwa wingi kwa kushirikiana na wakulima lengo likiwa ni kuongeza tija sambamba na thamani ya zao hilo nchini.

“Ufanisi wa uzalishaji wa zao hili umeongezeka baada ya serikali na AMDT kutia mkono na wanaendelea kutoa mafunzo na elimu ya shamba darasa kwa zaidi ya wakulima wengine 150.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *