Wakuliwa waaswa kilimo cha umwagiliaji matone
WAKULIMA wameaswa kujikita katika teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji wa matone ili kuleta matokeo chanya katika shughuli zao za kilimo hasa mabazo ya maharagwe, mahindi na alizeti
Mimea huitaji unyevu unyevu katika ukuaji wake tofauti na dhana iliyojengeka kwa wakulima wengi kuwa msimu wa masika ndiyo muda sahihi wa kuotesha mazao na kutarajia kupata mazao mengi
Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuboresha mifumo ya masoko ya kilimo nchini (AMDT) Charles Ogutu wakati wa ziara kutembelea mashamba darasa ya mfano yanayo zalisha mazao hayo katika Wilaya za Babati mkoani Manyara.
Tumekuwa tukipoteza rasilimali ya maji nchini bila kuitumia ipasavyo kwa kumwagilia mazao shambani hasa kunyeshea sehemu zisizo na mimea, kuja kwa teknolojia hii ya umwagiliaji wa matone katika shina la mimea itakuwa mkombozi kwa wakulima kwani huleta matokeo chanya kwa kupata mazao bora na hupunguza gharama.
Hivi karibuni tulifanya ziara ya kimafunzo nchini Zambia kuona wenzetu wamewezaje kufanikiwa katika teknolojia hii ya kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone ambapo mimea hupandwa katika mifereji ya maji tofauti na hapa nchini ambapo wakulima wengi hupanda miche juu ya matuta na kuupa mmea kazi ya kutafuta maji, alisema `Ogutu’.
Kwa upande wake ofisa kilimo wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Sebastian Joseph amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wakukima walionesha nia ya kuingia katika kilimo cha umwagiliaji kutoka katika vijiji vya Singe,Nakwa,Maghati, Gedamar na Galapo vilivyopo Babati Manyara baada ya kupatiwa mafunzo na kampuni ya uzalishaji mbegu bora ya Beula wakishirikiana na AMDT.
Lengo kubwa ni kuzidi kutoa elimu kwa wakulima wa mazao haya ili walime katika kipindi chote cha mwaka na kuwapatia kipato cha ukakika “Tunaendelea kutoa elimu ya namna bora ya kilimo cha umwagiliaji, kutipia mafunzo ya shamba darasa ya mfano kwa wakulima”
Safari Yahhi ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo ya teknolojia ya kilimo cha umwagilijai wilayani Babati mkoani Manyara, amekuwa mfano wa kuigwa baada ya kuwa mstari wa mbele katika kilimo maharage na mahindi.
Ameiomba serikali na wadau hao wa kilimo kuwasaidia kupata sola kwa ajili ya kuwapunguzia gharama za kununua mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji.