Wakuu wa Majeshi Malawi wawasili kushiriki CDF Trophy

DAR ES SALAAM: Timu ya Golf ya Jeshi la Malawi ikiongozwa na Wakuu wa majeshi wastaafu imewasili Katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Dar es Salaam Kushiriki Shindano la “NMB CDF TROPHY 2023”.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nahodha wa Timu hiyo Brigedia Jenerali Kondwani Kalino amesema wamekuja wachezaji 22 wakiwemo Wakuu  wa Majeshi wastaafu Jenerali Vincent Nundwe na Jenerali Henry Odillo

“Tumejipanga kucheza vizuri mchezo wa Gofu ni imani yetu tutashinda”amesema brigedia Jenerali Kondwani Kalino

“Mchezo ni afya mazoezi lakini kufurahi pia ni tumefanya mazoezi ya kutosha tupo kwenye mashindano.”Jenerali Vincent Nundwe Mkuu Wa Majeshi Mstaafu Malawi.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema wameipokea timu hiyo Kutoka Malawi na maandalizi yamekamilika na Mshindi atajipatia Zawadi ya Pikikipi, amesema Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo”

Shindano la Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF TROPHY 2023″ litaanza kutimua vimbi kesho Kwa Wachezaji wa ridhaa na Kufungwa Septemba 3,2023 huku zaidi ya Wachezaji 170 wakiwa wamethibisha Kushiriki.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button