Wakuu wa Wilaya watakiwa kuwa watiifu

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewaapisha wakuu wapya wa wilaya za Arusha, Longido na Arumeru na kuwaasa kuwa watiifu katika utumishi.

Hafla ya uapisho huo imefanyika leo jijini Arusha, ambapo walioapishwa ni Felicia Mtahengerwa (Arusha), Marko Ngu’mbi (Longido) na Emmanuela Mtatifikolo (Arumeru).

 

Amesema katika safari za maisha lazima uweke akiba unaweza kukutana na mtu popote pale, akiwasihi wakuu wapya kuwa watiifu katika utumishi wao na poa watiifu kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema nafasi ya ukuu wa wilaya ni nzuri endapo hekima zitatumika, huku akiwasihi wasiwe wavivu kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa dini na kimila.

“Kwani nani asiyejua wewe ni kiongozi msijitapetape sana, simamieni mambo sahihi, linalohitaji kusema sema au toa maelekezo, kwani kila wilaya za Arusha zina mambo yake mkifika katika wilaya zenu kuna mambo mtayakuta,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button