Wakwepa kodi Kagera kuundiwa kikosi maalum

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amesema uongozi wa mkoa umeungana na Mamlaka ya Mapato (TRA) na taasisi nyingine za wafanyabiashara mkoani Kagera kutafuta njia bora za kuunda kikosi maalumu ambacho kitakabiliana na wafanyabiashara sugu ambao wamekuwa kero kulipa kodi.

“Nachukua nafasi hii kuwaponageza wafanyabiashara mkoani Kagera ambao mmekuwa mkilipa kodi kwa hiari,bila shaka mnaona faida nyingi sana za kulipa kodi, maendeleo ni makubwa ukilinganisha na miaka iliyopita ,nawapongeza TRA Kagera kwa weledi mkubwa.

” alisema Mwasa

Akitoa taarifa za makusanyo ya kodi kwa miaka tofauti, Meneja wa TRA Kagera alisema mkoa huo umeendelea kupiga hatua na kuvuka asilimia kubwa ya kiwango kinachokusanywa na ndani ya robo ya mwaka wa fedha 2023/2024 asilimia 98 ya makusanyo imefanikiwa.

Alisema kuwa mahusiano ya wafanyabiashara na wafanyakazi wa TRA yamehimarika ,na ulipaji wa kodi kwa hiari umeongezeka na hakuna fungafunga ya maduka ya wafanyabiashara huku elimu ya kulipa kodi ikieendelea kutolewa kila mara kwa wafanyabiashara.

Kwa niaba ya Kamishina Mkuu wa TRA Makao Makuu, Ramadhan Sengati alisema kuwa tatizo la kutumia mianya ya vochochoro kukwepa kodi katika Mkoa wa Kagera bado ni kubwa sana ,shughuli za magendo na wafanyabiashara wanaotumia ziwa Victoria kutorosha bidhaa au kuingiza bidhaa kinyume na sheria bado ni kubwa sana hivyo serikali inapaswa kuongeza nguvu katika kikosi kinachoundwa na mkuu wa mkoa.

Hata hivyo alisema kuwa ujio wa meli ya mizigo itakayofanyasafari zake katika ukanda wa nchi za Afrika mashariki kupitia Ziwa Victoria itaongeza wigo wa makusanyo kwani ukosefu wa meli kubwa ya Mizigo imekuwa changamoto kubwa kwa nchi zilozouzunguka mkoa wa Kagera kushindwa kuleta bidhaa na kulipia kido hivyo mkoa kutopata mapato makubwa.

Habari Zifananazo

Back to top button