Walalamikia mitaro ya maji machafu Mpanda

MWENYEKITI wa Mtaa wa Rungwa, Kata ya Kazima Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi,  Mwelela Nkokwa, amesema suala la mitaro ya maji bado ni kero katika eneo lake na inashindwa kuhimili na kutiririsha maji kwenye makazi ya watu.

Akizungumza na HabariLEO  Mwenyekiti huyo, amesema anaumizwa kuona wananchi wake wakiteseka wakati suala la mitaro ameshalifikisha ofisi ya wilaya.

Amesema katika mkutano wa hadhara wa uliofanyikaFfebruari 21, 2023, wakati akisikiliza kero za wananchi na wafanyabiashara wa soko la Kababaye Kata ya Kazima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf, alitoa siku mbili wataalamu kutoka TARURA wafike na kufanya upembuzi, ili ukarabati ufanyike kuwanusuru wananchi, lakini anadai hadi leo hakuna mtu aliyefika.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Rungwa, wameeleza kuchoshwa na ahadi isiyotekelezeka ya kutengeneza mitaro itakayopitisha maji kutoka barabara kuu.

“Chanzo cha maji haya ni kukosekana mitaro, tunaomba mtusaidie kutuwekea mitaro la sivyo mtakuta siku moja tunaelea, kwa sababu wengine tuna watoto wadogo unaweza kwenda sokoni kujitafutia riziki ukarudi na kukuta kamesombwa na maji,” amesema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Martha.

 

Mwenyekiti wa Mtaa Rungwa,Mwelela Nkokwa,

Kwa upande wake Meneja TARURA Wilaya ya Mpanda, Joseph Kahoza amesema Sh milioni 450 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa mifereji ya mawe katika maeneo korofi Mpanda Mjini

Habari Zifananazo

Back to top button