Walete waletee! Simba Vs Yanga

DAR ES SALAAM: Mchakamchaka wa Ligi Kuu ya Wanawake utaendela leo ambapo miamba miwili katika ligi hiyo Simba Queens na Yanga Princess itaumana vikali katika Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo wa mwisho timu hizo zilikutana kwenye nusu fainali ya ngao ya jamii 2023 ambapo Simba Queens waliibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare.

Mpaka sasa timu hizo zimecheza michezo miwili na kujikusanyia alama sita katika michezo hiyo.

Michezo 12 ya mwisho timu hizo kukutana Simba Queens imeshinda michezo saba, huku Yanga Princess wakisajili ushindi katika mchezo mmoja pekee na sare zikipatikana mara nne.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button