Walete…waleteee kwa Mkapa!

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 4,2023, amekagua ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, ikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kuanza kwa michuano ya African Football League.
Majaliwa amejionea jinsi maeneo mbalimbali ya uwanja huo yanavyoendelea kufanyiwa ukarabati.
Katika ukaguzi huo Waziri Mkuu ameongozana na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro pamoja na viongozi mbalimbali.
Uwanja wa Mkapa utatumika katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League ambapo Simba itacheza dhidi ya Al Ahly ya Misri Oktoba 20 mwaka huu.