Walia na uchakavu wa miundombinu sokoni

TANGA: Wafanyabiashara wa soko kuu la Mgandini Jijini Tanga wameiomba Halmashauri ya Jiji la Tanga kuwaboreshea miundombinu ya soko ili kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri.

Wakiongea wakati wa kikao chao na Mkurungenzi wa Jiji hilo Said Majaliwa cha kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Walisema uchakakavu wa miundombinu ikiwemo mifumo ya majitaka imekuwa ikihatarisha hali za afya za wafanyabiashara hao pamoja na watumiaji wengine wa soko hilo Kwa ujumla.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Elizabeth Sozi amesema kuwa licha ya kutozwa ushuru na halmashauri hiyo lakini swala la miundombinu limekuwa changamoto sana hasa nyakati za mvua.

“Nyakati za mvua hapa sokoni huwezi kuuza kwani miundombinu ni chakavu tunaomba tuboreshewe ili tuweze kufanya biashara mahali pazuri”amesema.

Hata hivyo Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Said Majaliwa alisema soko hilo lipo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuwa la kisasa.

“Niwaombe wafanyabiashara tuwe na subra kwani serikali imeshaleta kiasi cha Sh bilioni nane kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu na ukarabati mwingine katika soko hilo”alisema Mkurungenzi huyo.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button