Walimu kortini kwa kufyatua vyeti feki

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Arusha, imewakamata na kuwafikisha mahakamani walimu wawili wa shule ya Sekondari ya Arusha (Arusha Secondary), kwa tuhuma za kutengeneza vyeti feki vya kidato cha nne.
Taarifa zinadai walimu hao, Salimu Nyetu ambaye ni Makamu Mkuu wa shule pamoja na mwalimu wa taaluma Raphael Swai, walikamatwa mwisho wa wiki shuleni hapo na kiasi cha sh,100,000, ikiwa ni sehemu ya malipo ya Sh 400,000, baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa Takukuru mkoani hapa.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, James Ruge alithibitisha kushikiliwa na kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa hao, ingawa hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa vile limeshafikishwa mahakamani.
 
” Ni kweli wamekamatwa na wameshafikishwa mahakamani na siwezi kuongea zaidi kwa kuwa liko mahakamani,”alisema Ruge.

Habari Zifananazo

Back to top button