Walimu, wasimamizi watakiwa kufuatilia ufundishaji shuleni

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI ayesimamia elimu, Dk Charles Msonde amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na wasimamazi wa elimu kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji shuleni na kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza wanamudu stadi ya Kusoma, kuandika na kuhesabu.

Ametoa maagizo hayo leo Aprili Mosi alipokutana na walimu wakuu, maafisa elimu na viongozi wanaosimamia elimu katika Mkoa Songwe kwa ajili ya kuhimiza utendaji kazi na utekelezaji wa mikakati ya serikali ya uboreshaji wa utoaji elimu nchini.

Dk Msonde amewaagiza wakuu wa shule kuwabainisha wanafunzi wote wa kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la nne wasiomudu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu na kuwawekea mkakati wa kuwasaidia ndani ya muda mfupi kabla yahawajaendelea na masomo mengine.

Advertisement

“Tuhakikishe wanafunzi wote wa darasa la kwanza wajue Kusoma, kuandika na kuheshabu, wakishaingia darasa la pili wanafundishwa kuongeza kasi wakati wa kusoma na kuandika lakini wakifika darasa la tatu ndio tunawapa Msingi wa kushika masomo mbalimbali na sio tena kusoma na kuandika” amsema Dk Msonde.

Aidha, Dk Msonde amewata walimu wakuu na wasimamizi wa ngazi zote kuondokana na hali ya kufanya kazi kwa mazoea na kuanza kivingine katika mwaka huu wa 2023 na kuhakikisha yasiyowezekana yanawezekana.