Walinda amani kuondoka DR Congo

WANAJESHI wa mwisho wa kikosi cha Kanda ya Afrika Mashariki wanaondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zaidi ya mwaka mmoja tu baada ya kutumwa kutuliza ghasia za waasi Mashariki mwa nchi hiyo.

Kikosi hicho ambacho kilijumuisha wanajeshi kutoka Kenya, Uganda, Burundi na Sudan Kusini kilianza kuondoka mapema mwezi huu baada ya serikali ya Congo kukataa kurejesha mamlaka yake, kwa sababu ya wasiwasi juu ya ufanisi wake.

Kamanda wa kikosi hicho, Meja Jenerali Alphaxard Kiugu alinukuliwa siku ya Alhamisi na gazeti la The East African akisema kuwa kikosi hicho kilitimiza wajibu wake licha ya propaganda mbaya walizokabiliana nazo.

Aidha alionya juu ya hatari ya makundi yenye silaha, likiwemo kundi la waasi la M23 kutumia pengo lililoachwa na kuondoka kwa kikosi hicho.

Wanajeshi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanatazamiwa kuchukua nafasi ya jeshi la Afrika Mashariki

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button