Walinda amani wa UN kuondoka DR Congo Desemba 2024

WALINDA amani wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo wataondolewa wote kufikia Desemba 2024. Umoja wa Mataifa unasema.

“Baada ya miaka 25 ya uwepo wa MUNUSCO rasmi wataondoka na na hakuna baadaye zaidi ya ifikapo mwisho wa 2024, Bintou Keita, kiongozi wa zoezi hilo ameeleza.

Amesema kuondoka kwa wanajeshi hao nchini humo kutakuwa na tripu tatu.

Advertisement

Baadhi ya wanajeshi walinda amani nchini DR Congo wameondoka mwishoni mwa mwaka jana.