Walioachiwa kwa msamaha wadakwa Tanga kwa uhalifu

JESHI la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia watu 8 ambao ni wahalifu waliotoka jela kutokana na msamaha baada ya kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha.

Kamanda wa Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe, amesema watu hao  ambao inaelezwa kuwa ni wahalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji wakutumia silaha, waliachiwa Magereza kutoka kwenye vifungo kutokana na msamaha.

“Tunawashikilia watu nane ambao wana makosa mbalimbali ikiwamo uporaji wa kutumia silaha na wengine wanatafutwa katika mikoa ya jirani, wapo ambao walimaliza vifungo gerezani, wahalifu hawa ndio waliovunja duka la simu Barabara ya 8 hivi karibuni na kuiba, “alisema Kamanda Mwaibambe na kuongeza:.

“Niwaombe Wananchi washerekee sikukuu kwa amani na wajiepushe na vitendo visivyofaa hususani hhalifu na uvunjifu wa sheria za barabarani.”

Habari Zifananazo

Back to top button