Waliofariki ajali Moro watajwa, wapo wanandoa

WATANO watano waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro wametambuliwa wakiwemo mume na mke, ambao pia ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro , Fortunatus Musilimu alisema  ajali hiyo ilitokea usiku wa Desemba 26,2022, eneo la  Iyovi,  Kata na Mikumi, wilayani Kilosa, ikihusisha  gari ndogo aina ya  Toyota  Allion  yenye namba IT 6954DNN, iliyogongana uso kwa uso na  kwa uso na gari kubwa la mafuta  aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili RAE 518C yenye tela  namba  RL 2686.

Amesema gari ndogo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma, ilikuwa ikiendeshwa na Festo Eliuzima Shoo  na gari kubwa  lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Morogoro lilikuwa likiendeshwa na Muthoni Richard raia wa Rwanda.

Musilimu alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo, kutaka kuyapita magari mengine bila tahadhari, ndipo wakakutana uso kwa uso, ambapo dereva huyo wa gari ndogo ni miongoni mwa waliofariki.

Wengine ni Grayson  Ng’obo mkazi wa Mbeya na Janeth John Luvanda (40), ambao kwa mujibu wa Kamanda huyo taarifa walizopata Grayson na Janeth ni mume na mke.

Marehemu Grayson  Ng’obo na mkewe Janeth John Luvanda enzi za uhai wao.

Aliwataja wengine waliofariki dunia ni Oswald John Luvanda (42) mkulima na  mkazi wa Mbeya, ambaye ni ndugu wa Janeth Luvanda  na John Davis Haule (37) Mwalimu wa shule ya Wanging’ombe iliyopo mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kanda ya  ya Mbeya umetoaa taarifa kuwa  Grayson Ngogo na Janeth Luvanda waliofariki kwenye ajali hiyo ni wanafunzi wa chuo chao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wanafunzi hao walifariki kwenye ajali iliyotokea mkoani Morogoro na kuwa  taratibu nyingine zitaendelea kutolewa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x