Waliofariki ajali ya Dodoma wafika saba
IDADI ya watu waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha Basi la Arusha Express na Lori katika eneo la Mzakwe Dodoma imefikia saba.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo alipowatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Waziri Ummy amesema kuwa watu tisa kati ya 21 waliopokelewa katika hospitali hiyo wameruhusiwa kutoka hospitalini na 11 wanaendelea na matibabu.
Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea vyema na matibabu.
Ummy amewashukuru watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea.