Waliohamia Msomera wafurahia kilimo

Waliohamia kwa hiari Msomera, mkoani Tanga wameanza kujionea fursa zilizopo katika kilimo na kulima mazao ya aina mbalimbali , tofauti na hali ilivyokuwa awali ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro

Baadhi ya wakazi hao wanaoishi Msomera kwa sasa, wanasema awali walipokuwa ndani ya hifadhi hawakuruhusiwa kulima wala kufanya shughuli zozote katika eneo hilo, lakini walipofika Msomera, Novemba 2022 mambo ni tofauti.

Mkazi wa Msomera, Jackson Kipuyo anasema katika eneo hilo analima,  kwani eneo hilo wana amani, uhuru na mipaka kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo cha umwagiliaji na cha kawaida kinachowapa mazao ya kutosha.

“Tumebadilika kimawazo na mtazamo maana hapa tunalima na kuvuna kule Ngorongoro haturuhusiwi kulima kwa sababu ya uhifadhi na kilimo hiki kimesaidia watoto kujua maana halisi ya mazao mbalimbali yanavyolimwa, kupandwa na kuvunwa na tumefurahi sana sana kuona mazao halisi shambani,” amesema.

Baadhi ya watoto wakizungumza na HabariLEO kwa kwanyakati tofauti,  ambao ni Meshack Joshua na Theresia Ndemgei wamesema wakiwa Ngorongoro hawakuwa wakilima wala kujionea uhalisia wa mazao yanavyoandaliwa mashambani na kupandwa hadi kuvunwa, lakini sasa wamejionea.

“Tulipokuwa Ngorongoro hakujua hata kushika jembe au kulima kilimo cha umwagiliaji, lakini hapa Msomera tunalima kwa mikono yetu wenyewe na kujionea aina mbalimbali za mazao yanayovunwa ambayo hatukuwahi kuyaona awali,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button