Waliokosa fursa ya kuendelea na masomo wafikiwa

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Furahika limepokea Sh milioni 200 kwa ajili ya kuendeleza mradi wa Elimu Bure kwa watoto na vijana wenye umri kuanzia miaka 13 hadi 24 ambao wamekosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia, mimba na kufeli darasani.

Usajili kwa ajili ya kuandikisha wanaotaka kujiunga na masomo hayo ya ufundi umeanza katika chuo hicho na unatarajiwa kukamilika Januari 28 kabla ya kuanza kwa mafunzo ya kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho chenye usajili namba VET/DSM/PR/2021/D169, Dk David Msuya amesema elimu inayotolewa hapo ni ya bure na vijana wanaowapokea ni wale walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali.

“Vijana tunaowapokea kwa ajili ya masomo ni wale walioshindwa kuendelea na shule kwa kupata alama hafifu katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha pili na nne ama kushindwa kulipa ada, hapa tunawakaribisha ili watimeze ndoto zao na kuepuka utegemezi,” amesema Dk Msuya.

Ameongeza kuwa kituo hicho kazi yake ni kuwapokea vijana na kuwasaidia kuwapa ujuzi wa fani mbalimbali ikiwemo kozi ya Utalii, Hotel Management, Ushonaji, IT na nyinginezo zitakazowasaidia kupata ajira ama kujiajiri wenyewe ambapo Januari 2024 wataanza kufundisha kozi mpya ikiwemo ufundi wa pikipiki, uchoraji wa ramani za majumba, upishi, ufundi uwashi na muziki.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button