Waliokufa Gaza wafikia 20,000

IDADI ya watu waliofariki kutokana na vita katika Ukanda wa Gaza imefikia 20,000, mamlaka nchini Palestina imeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa Al-Jazeera imeeleza takriban watoto 8,000 na wanawake 6,200, ni miongoni mwa waliokufa, mtandao wa Al Mayadeen wa Lebanon umesema wahudumu wa afya 310 na waandishi wa habari 97 wameuawa pia.

Tangu kuporomoka kwa makubaliano ya siku saba ya usitishaji wa vita hivyo mnamo Desemba 1, vita vimeingia katika hatua kali zaidi na mapigano ya ardhini.

Advertisement

Taarifa hiyo imeongeza kuwa uvamizi huo umesababisha watu 52,600 kujeruhiwa, huku wengine 6,700 wakiwa bado wamepotea chini ya vifusi au kusikojulikana hatima yao, asilimia 70 kati yao ni watoto na wanawake.

1 comments

Comments are closed.