Waliokufa kimbunga Marekani wafikia 26

IDADI ya waliopoteza maisha kutokana na vimbunga nchini Marekani imefikia 26 hasa katika miji na majiji yaliyopo Kusini na Magharibi mwa taifa la hilo.

Imeelezwa kuwa katika dhoruba hiyo, nyumba ziliharibiwa na maelfu ya watu kuachwa bila makazi pamoja na kusababisha uharibifu katika majimbo ya Arkansas, Tennessee, Illinois, Indiana, Alabama na Mississippi yote yamerekodi vifo .

Advertisement

Zaidi ya ripoti 50 za awali za kimbunga zilirekodiwa Ijumaa katika majimbo saba, ikiwa ni pamoja na huko Arkansas, ambapo kimbuka hiko kiliua watu watano, wanne katika mji mdogo wa Wynne na mtu mwingine huko North Little Rock, maafisa wa eneo hilo walisema.

Watu watatu waliuawa huko Indiana usiku na kwamba kulikuwa na uharibifu wa nyumba na idara ya zima moto ya kujitolea karibu na Sullivan, jiji la umbali wa maili 95 kusini magharibi mwa Indianapolis, Polisi wa Jimbo Sgt. Matt Ames alisema.

Zaidi ya watu 34,000 katika jimbo hilo hawakuwa na umeme Jumamosi alasiri, kulingana na tovuti ya kufuatilia poweroutage.us.

/* */