Waliokufa mafuriko Somalia wafikia 96

IDADI ya watu waliofariki kutokana na mafuriko Somalia imepanda hadi 96, Shirika la Habari la Serikali SONNA limeripoti.

“Idadi ya vifo vya mafuriko ya Somalia imepanda hadi 96,” SONNA ilieleza, na kwamba takwimu hiyo imethibitishwa na Mahamuud Moallim, Mkuu wa Wakala wa Kudhibiti Majanga nchini humo.

Mafuriko hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa na yamesababisha takriban watu 700,000 kuyahama makazi yao katika eneo zima la Pembe ya Afrika, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button