Waliokuwa kwenye nyambizi Titan waaga dunia

Kampuni ya Ocean Gate imethibitisha muda huu kuwa watu wote watano waliokuwa kwenye nyambizi ya Titan wamefariki dunia.

Taarifa hiyo imekuja huku walinzi wa Pwani wa Marekani wakisema kuwa mabaki ya nyambizi yamegundulika.

Msako wa kuitafuta nyambizi, ambayo ilitoweka Jumapili baada ya kuanza kazi ya kukagua mabaki ya meli ya Titanic, ulikuwa ukilenga katika eneo ambalo ndege za Canada ziligundua “kelele za chini ya maji” Jumanne na jana.

Advertisement

Maafisa wa walinzi wa Pwani ya Marekani walikadiria kuwa abiria hao watano wanaweza kukosa hewa kabla ya saa 7:10 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki leo, na eneo la meli iliyopotea limesalia kuwa kitendawili.

“Sasa tunaamini kwamba Mkurugenzi Mtendaji wetu Stockton Rush, Shahzada Dawood na mwanawe Suleman Dawood, Hamish Harding, na Paul-Henri Nargeolet, wameaga dunia.” imeeleza taarifa hiyo.