Waliouawa Gaza wafikia 198
TAKRIBANI watu 198 wameuawa na 1,610 kujeruhiwa katika eneo la Wapalestina huko Gaza wakati wa kulipiza kisasi kwa Israeli baada ya shambulio la vikosi vya Hamas nchini Israeli, Wizara ya Afya imesema.
–
Idadi ya wahanga inayoongezeka inakuja baada ya kundi la Wapalestina wanaoendesha Ukanda wa Gaza kufanya shambulio kubwa zaidi kwa Israel kuwahi kutokea kwa miaka mingi.
–
Huduma ya kitaifa ya uokoaji nchini Israel imesema takribani watu 100 waliuawa na mamia kujeruhiwa, na kuwa shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Israel kwa miaka mingi.
–
Idadi isiyojulikana ya wanajeshi na raia wa Israel pia walikamatwa na kupelekwa Gaza.
–
Hamas ilisema mapigano ya bunduki yalikuwa yakiendelea katika maeneo kadhaa ndani ya Israel.
–
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant alionya Hamas ilifanya “kosa kubwa” katika kuanzisha shambulio hilo, ambalo lilianza saa 6:30 asubuhi kwa saa za huko (03:30 GMT) na kuhusisha misururu ya makombora yaliyorushwa kutoka maeneo mengi huko Gaza.
–
“Tuko vitani, adui atalipa thamani ambayo haijawahi kushuhudiwa.” Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema katika ujumbe wake wa video kutoka makao makuu ya kijeshi mjini Tel Aviv.
–
Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya Gaza kujibu mashambulizi hayo. “Mamia ya ndege za kivita za jeshi la Israel kwa sasa zinalenga kundi la kigaidi la Hamas katika Ukanda wa Gaza,” ilisema.
–
Mohammed Deif, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Hamas, alisema ufyatuaji wa roketi uliashiria kuanza kwa “Operesheni Al-Aqsa mafuriko”, na alitoa wito kwa Wapalestina kila mahali kupambana na uvamizi wa Israel.
–