MKUU wa Wilaya ya Chato, Martha Mkumpasi, ameagiza ufanyike msako wa wazazi waliozuia watoto kujiunga na kidato cha kwanza na wanaobainika wakamatwe na kutozwa faini ya mifuko ya saruji kwa ajili ya shule.
–
Mkumpasi ametoa maagizo hayo Januari 18, 2023, baada ya kutembelea na kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza, shule ya sekondari Sumaye-Buziku iliyopo Kata ya Buziki wilayani Chato.
–
Amesema bado kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hawajaripoti shule wilayani humo, ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi waliofaulu hivyo ni lazima hatua zichukuliwe.
–
“Naagiza watendaji wote wa vijiji, watendaji wa kata, na viongozi wote wa chama tushirikiane kuwasaka wazazi ambao bado wanawashikilia watoto majumbani, ” amesema na kuongeza;
–
“Ninaagiza wazazi wote wanaokiuka amri hii tuweze kutoa adhabu ambazo ni za kijamii, wanunue mifuko ya simenti, ije ijenge madarasa hapa.”
–