‘Walipeni fidia wanaopisha miradi Mchuchuma, Liganga’

Mradi wa Makaa ya Mawe, Mchuchuma

KAMATI ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeagiza serikali kulipa fidia ya wananchi waliopisha miradi ya chuma na makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Akitoa maagizo hayo baada ya kikao na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, David Kihenzile alisema mradi huo ni wa miaka 124 iliyopita na umekuwa ukiimbwa bila kutekelezwa.

“Mradi huu sasa uanze kutekelezwa na wananchi walipwe fidia za kupisha mradi mwaka huu,” alisema.

Advertisement

Alisema dhamira ya kamati ni kuona mradi huo wa Mchuchuma na Liganga unaanza kutekelezwa na kwamba mradi huo ni miongoni mwa miradi 17 ya kimkakati.

Alitaja mradi mwingine kuwa ni wa magadi soda mkoani Arusha na wa Eneo Huru la Kibiashara wa Bagamoyo.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya kamati kupanda bei ya bidhaa mbalimbali, Kihenzile alisema haikuwa sehemu ya mjadala wao, lakini wao kama wabunge wameishauri serikali iweke mikakati ya kushusha bei za bidhaa ili kuwasaidia wananchi.

Naye, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaudi Kigahe alisema wizara hiyo imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati mitatu kwa kamati hiyo ukiwemo huo wa Liganga na Mchuchuma.

Kuhusu suala la fidia kwa wananchi wa Liganga na Mchuchuma, Kigahe alisema wanaangalia namna ya kulipa fidia kwa wananchi hao pamoja na kumpata mwekezaji mahiri awekeze ili ku