Walter Harison: Pacome yupo kamiligado

DAR ES SALAAM: MENEJA wa Klabu ya Yanga, Walter Harson amesema kiungo wa timu hiyo, Pacome Zouzoua yupo tayari kutumika katika michezo iliyosalia ya Ligi Kuu.

Yanga imebakisha michezo sita kabla ya ligi kumalizika ikiwa nafasi ya kwanza ambapo wameshakusanya pointi 62 katika michezo 24.

Akizungumza na HabariLEO mapema leo, Walter Harison amesema kwa sasa Pacome raia wa Ivory Coast yupo tayari kutumika ambapo alipata dakika chache za kucheza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United.

“Kuhisiana na kucheza michezo ya ligi kuu hakika tunategemea mmoja wa watu ambao tunagemea kuwatumia kwenye michezo hiyo,”amesema Walter.

Amesema kocha hakutaka kuhatarisha afya ya mchezaji huyo kwa kumuwahisha uwanjani hivyo alipewa muda wa kuendelea kupona taratibu.

Meneja huyo amesema tetesi za kutokuwepo kikosini mchezaji huyo kuhusishwa na masuala ya madai ni taarifa zinazopaswa kupuuzwa na kwamba hakuna ukweli katika hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button