Wamiliki kumbi za starehe kuwa na vibali

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wamiliki wa kumbi za starehe kujisajili na kupata kibali cha kuendesha biashara zao.

Akizungumza leo Katibu Mtendaji wa Basata, Dk Kedmon Mapana amesema baraza ni shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019.

Amesema kufanya usajili na Basata kwa kumbi za starehe ni muhimu kwa sababu za msingi kuzingatia sheria na kanuni usajili na Basata husaidia kumbi za starehe kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia shughuli za burudani.

“Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa kumbi hizo zinafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za usalama, afya, na burudani zilizowekwa na mamlaka husika.”

“Kupata Vibali na RuhusaUsajili na BASATA hufanya iwe rahisi kwa kumbi za starehe kupata vibali na ruhusa zinazohitajika kwa ajili ya kufanya shughuli za burudani. Hii ni pamoja na vibali vya kufanya maonyesho ya moja kwa moja, vibali vya matangazo, na vibali vingine vinavyohitajika kulingana na aina ya biashara,” amesema

Habari Zifananazo

Back to top button