Wamiminika kutoa maoni mitaala ya elimu nchini

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema kuwa tayari watu zaidi ya 200,000 wameshatoa maoni  kuhusu mtaala mpya wa elimu huku ukurasa wa maoni ukitarajiwa kufungwa rasmi Mei 31,2023.

Aidha mtaala mpya wa elimu unatarajiwa kuanza kutekelezwa January,2024 ambapo miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa ni pamoja na elimu ya lazima kuwa miaka 10 huku elimu ya msingi kuishia darasa la sita na elimu ya sekondari kwa miaka minne.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Kuzindua kamati ya Ushauri wa Kiviwanda ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambayo itashauri kuhusu mitaala ,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof James Mdoe amesema Katika kukuza Sekta ya Elimu ya juu serikali imefanya juhudi kubwa na za dhati kuanzisha na kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu (HEET).

“ Kupitia mradi huu, serikali itaboresha mitaala, rasilimali-watu na mazingira ya kufundishia na kujifunza katika vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu 23 ili mfumo wetu wa Elimu ya juu ujikite zaidi katika kutoa Elimu Ujuzi ambayo itawafanya vijana wahitimu waweze kuzalisha ajira au kujiajiri,”alieleza.

Aidha amesema Mradi utaanzisha Kampasi 14 za Vyuo Vikuu katika mikoa ambayo ilikuwa haina Taasisi za Elimu ya Juu kwa kujenga Kampasi zitakazokuwa zinalelewa na Vyuo Vikuu kamili ambavyo vinatekeleza Mradi huu.

Habari Zifananazo

Back to top button