Wamshukuru Rais Samia kuwajengea mferejei kuzuia mafuriko

ZAIDI ya wakulima 370 wa mahindi, maharage na mbogamboga wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea mfereji na tuta kuzuia marufiko katika Halmashauri ya Mji mdogo wa Bonde la Kairo kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wa mazao hayo katika bonde hilo baada ya Taasisi ya Kuboresha Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT)inayo ongoza na Ofisa Mtendaji mkuu wake, Charles Ogutu kudhamini mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima kupitia Shirika la Agro Tanzania lililopo Njiro Arusha.

Mwitikio huo, umekuja kutokana na Rais Samia kuwezesha kuwachimbia mfereji na tuta linalozuia mafuriko katika Bonde la Kairo na hivyo kutoa fursa kwa wakulima kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji kutoka na visima katka mashamba yao.

Hayo yalisemwa na Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Agro Tanzania, Flora Marere wakati wa ziara yake na waandishi wa habari kutembelea shamba la mfano wa kilimo cha mahindi lililopo katika halmashauri hiyo jana.

Lengo kubwa ni kuzidi kutoa elimu kwa wakulima wa mazao haya ili walime mwaka mzima na kuinua kipato cha mkulima mmoja mmoja kwa kuuza mazao hayo na kujihakikishia kupata chakula cha uhakika katika kipindi chote cha mwaka.

“Tunaendelea kutoa elimu ya namna kuzalisha mbegu bora na kupata mazao yenye tija kupitia kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia visima vilivyopo katika mashamba, kutipia mafunzo ya shamba darasa yanayotolewa na taasisi za utafiti za mbegu bora na kuboresha kilimo cha mazao nchini”.

Awali mkulima wa zao la mahindi katika bonde hilo, Brison Mbuya alikuwa akivuna kati ya gunia tano hadi saba kwa ekari moja kabla ya kupatiwa mafunzo maalum ya shamba darasa, tofauti na sasa, ambapo anavuna kati ya gunia nane hadi kumi kwa kila msimu wa mavuno baada ya miezi mitatu kwa mwaka, alisema mkulima huyo, Mbuya.

Lengo ni kuhakikisha matumzi hayazidi mapato baada ya kuuza mazao yetu mwishoni mwa msimu, na hii ilisabaishwa na kukosekana kwa mbegu bora za kuzalishia mazao na kilimo cha kutegemea msimu wa mvua ambazo si za uhakika.

Pia tunalishukuru Shirika la Agro Tanzania na mdhamini wake Taasisi ya kuboresha mifumo ya masoko ya kilimo nchini (AMDT) kwa kusikia kilio cha wakulima wa bonde hilo kwa kuwapatia mashine za kisasa za kupandia mazao yao ambapo tumepata matokeo chanya kwa kupanda hekari tatu kwa siku tofauti na awali hekari moja kwa siku.

Habari Zifananazo

Back to top button