Wanafunzi 1,073,941 kujiunga kidato cha kwanza

WANAFUNZI 1,073,941 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

Hayo yamebainishwa leo mjini Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Angellah Kairuki, ambapo amesema wanafunzi hao wamechaguliwa kwenda shule za bweni na za kutwa.

Amesema kati ya wanafunzi hao  wasichana ni 559,095 na wavulana ni 514,846, wana sifa stahiki ya kujiunga na masomo ya sekondari.

Amesema kati yao waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza, wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,775 sawa na asilimia 0.26 ambao kati yao ni wavulana na 1,491 na wasichana ni 1,284.

Amesema uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza umefanyika kwakutumia mfumo wa kieletrooniki wa uchaguzi wa wanafunzi ulioundwa na wataalam wa Tehama wa Ofisi ya Rais Tamisemi na Baraza la Mitihani la Tanzania, ambapo mfumo huo umesaidia kupunguza muda wa uchaguzi wa wanafunzi, gharama kupunguza zinazotumika katika upangaji na uchaguzi wa wanafunzi.

Habari Zifananazo

Back to top button