Wanafunzi 20 kuweka kambi China

WANAFUNZI 20 kutoka Tanzania wamekwenda China kwa ajili ya kambi ya majira ya kiangazi kujifunza utamaduni wa kichina ambao utawahamasisha zaidi kusoma zaidi lugha hii.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Zhang Xiaozhen amesema hayo wakati wa kuwaaga wanafunzi hao.

Amesema ziara hiyo ya wiki mbili itahusisha wanafunzi kutoka shule mbili za sekondari ikiwemo St Christina na Baobab ambao watatembelea majiji ya Beijing, Jinhua na Shanghai.

Mkurugenzi huyo amesema wanafunzi hao watajifunza vitu mbalimbali pamoja na kuboresha lugha ya kichina katika maeneo mbalimbali.

“Ziara hii itawahamasisha wanafunzi kuelewa tamaduni mbalimbali pia itakuwa chachu ujifunzaji wao,” alisema.

Amesema wanafunzi wataweza kutofautisha na kulinganisha mambo ya msingi kati ya tamaduni ya nchi hizo.

“Ziara hii itawawezesha kutembelea vituo vitatu katika masuala ya siasa, uchumi na utamadui katika mji wa Beijig,

” Pia watatembelea vituo vya biashara na uchumi pamoja na miji mashuhuri ya Shanghai na Jinhua ambapo Chuo Kikuu cha Zheijiang kipo huko ” amesema.

Amesema ziara hiyo imekuja baada ya kushindwa kufanyika kwa muda kutokana na mlipuko wa Covid 19.

” Tulianza program hii mwaka 2017 kabla ya covid 19, tayari wanafunzi 81 wameshafanya ziara ya namna hii Nchini China kwenye majiji tofauti,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Shalia Mpenda kutoka sekondari ya Baobab amesema ziara hiyo itawawezesha kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa kichina ikiwemo lugha yao

Kiongozi wa ziara hiyo Goodness Mfanga amesema wanafunzi hao waliochaguliwa katika ziara hiyo wamekuwa wakijifunza kwa bidii hivyo watakuwa mabalozi wazuri kwa wanafunzi wenzao.

Mfanga ambaye pia ni mwailmu wa Baobab amesema mafunzo watakayopata kwenye ziara hiyo yataboresha uelewa wao katika kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika katika njia inayotakiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button