Wanafunzi 4000 safi kidato cha sita Tanga

Jumla ya wanafunzi 4451wamesajiliwa kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza kidato cha sita na uwalimu katika Mkoa wa Tanga

Hayo yamesemwa na Ofisa Elimu Mkoa wa Tanga, Newaho Nkisi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa watahiniwa hao watafanya mtihani katika vituo 44 vilivyoko katika wilaya 11 za mkoa huo.

Amesema kuwa kati ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ni 3962, huku waliosajiliwa vituo binafsi 239  huku wa uwalimu wakiwa ni watahiniwa 240.

Aidha amewataka wasimamizi wa mitihani hiyo kuwa makini ,wazalendo na  waadilifu na kuacha udanganyifu katika mitihani, kwani Kwa kufanya hivyo ni sawa na kosa la uhujumu uchumi.

“Niwaombe wasimamizi wa mitihani kuwa waadilifu kwa kudhibiti udanganyifu wa aina yoyote, ambao utafanywa na wanafunzi au kwa ushirikiano na walimu, ili kujenga taifa bora, “amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button