Wanafunzi 50 Kenya walazwa ugonjwa usiojulikana

WANAFUNZI 50 wa shule ya sekondari ya wasichana Eregi Girls High School nchini Kenya wamelazwa hospitalini katika mji wa Kakamega, baada ya kukumbwa na ugonjwa usiojulikana ulioowacha wanafunzi hao wakishindwa kutembea na kutetemeka mwili mzima.

Kwa mujibu wa mtandao wa NTV wa Kenya, baadhi ya wanafunzi walizungumza na mtandao huo Jumatatu na kueleza kuwa wanashindwa kusimama vizuri kwani wanakosa nguvu kwenye maungio ya miguu hata hivyo hawahisi maumivu.

Baadhi ya wazazi wameulaumu uongozi wa shule hiyo kwa kushindwa kutoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo hata hivyo hofu imetanda kwa baadhi ya wazazi na kuamua kuwarudisha nyumbani watoto ambao hawajaathirika na changamoto hiyo.

Baada ya agizo la kuifunga shule hiyo, Wizara ya Elimu, Ezekiel Machogu anatarajia kuzuru taasisi hiyo kujionea mazingira sambamba na kuzungumza na baadhi ya watumishi wa shule hiyo.

Taarifa ya Serikali ya Kaunti ilisema kuwa Bodi ya Usimamizi, Maafisa wa Wizara ya Elimu na Tume ya Kuajiri Walimu walifanya mashauriano kabla ya uamuzi huo kufanywa.

“Wanafunzi wa kidato cha 1, 2 na 3 waliruhusiwa kuvunja kwa muda na wanatarajiwa kuripoti wiki ijayo mara baada ya kutathminiwa kwa uangalifu na hatua za lazima ili kuzuia kujirudia kwa hali kama hiyo,” ilisema taarifa hiyo. kwa sehemu.

Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Kaunti ya Kakamega, Dk Steven Wandei alisema ugonjwa wa kuambukiza unaweza kuangamiza familia nzima ikiwa hautadhibitiwa vyema.

Habari Zifananazo

Back to top button