Wanafunzi 566,840 kuanza mitihani kidato cha nne
JUMLA ya watahiniwa 566,840 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne utakaoanza kesho Novemba 14, 2022 Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu Mtendaji wa Baraza la Mitihani ( NECTA), Athuman Amasi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mtihani huo.
Amesema watahiniwa 533,001 kati ya hao ni shule na 31, 839 wa kujitegemea .
Kati ya hao watahiniwa wavulana ni 247,131 sawa na asilimia 46.19 na wasichana 287,870 sawa na asilimia 53.81.
Amesema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwamo mitihani kufika kwenye mikoa na vituo husika.