Wanafunzi Chuo cha IAA wapania makubwa TEHAMA

ARUSHA: WANAFUNZI wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamepata fursa ya kuonesha ubunifu na uvumbuzi katika TEHAMA katika Kongamano la kimataifa la TEHAMA.
Kongamano hilo ambalo linawakutanisha wadau wa TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi lenye kauli mbiu ‘Mabadiliko ya Kidigitali katika kuendeleza shughuli za binadamu’.
Mkuu wa Chuo IAA, Prof. Eliamani Sedoyeka akizungumzia Kongamano hilo leo Novemba 8, 2023 amesema ili kuendana na kasi ya serikali katika uwekezaji kwenye TEHAMA, IAA imeendelea kuwekeza katika uboreshaji wa miundombinu na uanzishwaji wa mitaala bora.
Amesema lengo ni kutoa wataalam wenye uwezo wataokakubalika sokoni na watakaotumia elimu na ujuzi wao kutatua changamoto katika jamii.
“Sisi kama Chuo tumewekeza katika miundombinu ya TEHAMA, mitaala na rasilimaliwatu; IAA kupitia Mradi wa HEET tunatarajia kujenga kituo cha kikubwa cha umahiri cha TEHAMA, ambapo mtu yeyote atakayehitaji suluhisho la changamoto yoyote ya TEHAMA atakuja IAA,” amesema Sedoyeka.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini, Mkurugenzi wa Huduma za Kiufundi Mhandisi Jasson Ndanguzi amesema, Tume hiyo itaendelea kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu katika kufanya tafiti zinazoibua mwelekeo wa TEHAMA, zinazotatua changamoto za jamii, kuibua fursa za kiuchumi pamoja na kuiwezesha serikali kuandaa sera zinazoendana na wakati.
Naye Amidi wa Kitivo cha TEHAMA katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Edson Lubua amesema kongamano hilo limekuwa likitoa motisha kwa wanafunzi na kuonesha thamani ya kazi za bunifu zao pale wanapozionesha kwa walaji ambao ni makampuni, waajiri na taasisi mbalimbali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Marie Allen
Marie Allen
24 days ago

I get paid more than $140 to $170 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this (Ql)I have earned easily $25k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
.
.
.
Here is I started.…………>> http://Www.Smartcareer1.com

Julia
Julia
23 days ago

Everybody can earn 500 dollars daily. Yes! you can earn more than you think by working online from home. I have been doing this job for like a few weeks and my last week payment was exactly 30,000 dollars.
.
.
Detail Here—————————————————————>>> http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x