Wanafunzi Kimandolu wakabidhiwa sare za shule

DIWANI wa Kata ya Kimandolu, Abraham Mollel maarufu kwa jina la “Kobra ” amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi zaidi ya 100 wa Shule ya Msingi, Kimandolu Jijini Arusha ili kuongeza juhudi katika masomo.

Akikabidhi sare hizo leo, Kobra amesema sare hizo ni mchango wake kwa jamii katika kuleta chachu ya maendeleo ya elimu.

“Nimewaza nifanye nini kwa jamii yangu nikaona nigawe sare hizi kwa watoto hawa ili kuleta chachu katika elimu kwani wakivaa sare za shule zilizoisha na wengine uwezo mdogo nasononeka.”amesema Kobra.

 

Naye mmoja wa wanafunzi walionufaika na sare hizo, Zuwena Juma alimshukuru diwani huyo kwa kukumbuka wanafunzi ambao baadhi yao wanachangamoto mbalimbali za kimaisha

Habari Zifananazo

Back to top button