Wanafunzi milioni 1.7 kufanya mtihani la nne

DAR ES SALAAM; Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limetangaza tarehe ya kufanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa mwaka 2023, ambapo mitihani hiyo itaanza rasmi Oktoba 25 hadi Oktoba 26, 2023, huku ya kidato cha pili ikianza Oktoba 30 hadi Novemba 9, 2023.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24,2023 jijini Dar es Salam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dk. Said Mohamed, amesema jumla ya wanafunzi 1,692,802 wamesajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2023, ambao ni sawa na asilimia 94.

84, huku kidato cha pili waliosajiliwa kufanya mtihani huo wakiwa ni wanafunzi 759,573.


Pia baraza hilo limetoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia upimaji kufanya kazi yao kwa uadilifu, huku wamiliki wa shule binafsi wakitakiwa kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote wa mitihani hiyo.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button