Wanafunzi msingi wafundishwa kutengeneza ndege

ZAIDI ya wanafunzi 150 kutoka shule tatu za msingi za Twiga, Moringe na Sokoine zilizopo jijini Dar es Salaam wamefundishwa kutengeneza na kurusha ndege zisizo na rubani ‘Drones’.

Mafunzo hayo ya vitendo ya siku tatu  yametolewa na Taasisi ya Let Read Run and Drow ya nchini Marekani kwa kushirikiana Camara Education Tanzania kwa lengo la kuwasaidia katika masomo ya sayansi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Ofisa Miradi wa Camara Education Tanzania, Asia Bonanga amesema dunia imebadilika na kuna mabadiliko ya teknolojia yanaenda kasi, hivyo  lengo kubwa ni kuwasaidia wanafunzi kupata elimu ambayo itawasaidia siku za baadae.

“Na tunafahamu kuwa sasa ‘drones’ ni biashara inatumika katika kilimo kwenye sherehe mbalimbali, tunawapa haya mafunzo wakiwa wadogo ili waweze kutumia maarifa kwa manufaa,”amesisitiza.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Let Girls Read Run and Grrow, Idara Out amesema wanachojitahidi kufanya  ni kutoa ujuzi na wanafunzi wamefika katika kambi hiyo  katika mradi huo ambapo kuna  wanaotengeneza drones zao wenyewe na wengine wanatengeneza zilizoharibikana  na zinapaa.

“Kwa umri wao bado wanaweza kuwa mainjinia na somo la fizikia inaruhusi hili kutengeneza drone watakapofika vyuo vikuu wataendelea kujifunza kwa sababu wanajua na wamejengewa msingi,” amesema.

Kwa upande wake mwanafunzi aliyepata mafunzo hayo Abdulswamadi Poko amewashukuru walimu wake  kwa kumleta kujifunza jinsi ya kutengeza drones na pia waandaaji.

“Nawashukuru siku nikikutana na mtu aliyeharibikiwa drones naweza kumtengenezea na nitaendelea kujifunza zaidi,”ameeleza.

Habari Zifananazo

Back to top button