Wanafunzi sekondari wawafanyia mtihani la saba

Mwanza

MWANZA; Polisi  mkoani Mwanza inawashikilia na kuwahoji watu saba kwa tuhuma za udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba kwa kuwachukua wanafunzi wa sekondari na kuwafanyisha mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wa darasa la saba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema leo kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 13 mwaka huu katika Shule ya Msingi Igulumuki, Kata ya Igulumuki, Sengerema.

Amesema hayo yamebainika wakati Kamati ya Mitihani ya Wilaya ya Sengerema ilipotembelea shule hiyo kwa ajili ya ukaguzi na kubaini kufanyika kwa udanganyifu huo, ambapo mkondo namba mbili na tatu kulikua kumeingizwa wanafunzi wa sekondari watatu na kufanya mitihani ya darasa la saba.

Advertisement

 

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *