Wafanya udahili maonesho elimu ya juu

WANAFUNZI waliokatisha masomo yao nchini Sudan kutokana na sababu mbalimbali nchini humo wameanza kupata tumaini la kuendelea na masomo yao baada ya kufanya udaili kupitia Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Glabal Link ambao ni mawakala wa vyuo vikuu nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel alisema waliweza kupokea zaidi ya wanafunzi 43 ambao walikatisha masomo yao nchini Sudan wakiwa mwaka wa 3 na 4 kuomba kupatiwa nafasi ya kuendelea na elimu yao katika vyuo vingine.

Alisema ilibidi kufungua banda maalum kwaajili ya kuwasikiliza na kuwasaidia kupata vyuo ikiwa kuongea na vyuo wanavyoshirikiana navyo kutoka Uturuki, Uingereza, India nan chi zingine ili kuwapokea bila pingamiza huku wengine wakishauriwa kusoma hapa hapa nchini.

Advertisement

Kupitia banda hilo wamepokea raia wa Sudan wegine zaidi ya 193 wakihitaji kuunganishwa na vyuo vya ndani na nje ya nchi, kwaajili yao na ndugu zao ambao wapo nje ya nchi.

“Kwa mwaka huu ushirikiano ulikuwa mkubwa sana kati ya vyuo vya ndani kwa ndani, lakini mawakala wa vyuo vya nje na vyo vingine vya nnje vilivyoleta watu wao hapa nchini.” alisema.

Alisema kuisha kwa maonesho haya, watakuwa wakiendelea na udahili huo katika chuo chao mkoani Dar es Salaam, baada ya hapo watakuwa katika maonesho yoteikiwemo onesho la Nane nane, tamasha la Elimu Zanzibar na Malysia.

Mkurugenzi Udahili na Menejiment ya Data (TCU), Prof Charles Kihapa alisema mwaka huu katika maonesho ya 18 ya vyuo vikuu Tanzania, yaliudhuliwa na vyuo vikuu vya ndani ya nchi, mawakala wa vyuo vikuu na kutoka nje ya nchi.

“Tamasha limezidi kukua watu wamekuwa wakipata uelewa mkubwa sana, na tunashukuru wote ambao wamekuwa wakituunga mkono ikiwemo wadhamini na waandishi abao wanaowanafanya tuendelee kusikika na watu kuwepo hapa” alisema.

6 comments

Comments are closed.