Wanafunzi vyuo vikuu walaji wakubwa wa chips

WANAFUNZI wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam imeelezwa kuwa ndio walaji wakubwa wa chipsi.

Kutokana na hali hiyo ikitokea kwamba vyuo hivyo vimefungwa, hali katika masoko mbalimbali ya viazi vinavyotumika kutengeneza chakula hicho yanakwama na biashara inakuwa haiendi, kwani wateja hao ama wanarudi mikoani kwao au wapo nyumbani wanakula vyakula vingine.

Akizungumza na HabariLEO, mfanyabiashara wa  viazi katika Soko la Urafiki, George Nyangachi, amesema kutokana na uzoefu walionao, miaka yote msimu wa ufungwaji wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam unapunguza ununuaji wa viazi katika soko hilo na mengine yenye bidhaa hizo.

Advertisement

” Walaji wakubwa ni wanafunzi wa chuo kwa sababu vyuo vikifungwa biashara zetu zinadorora, wakifungua wanafunzi wa chuo ni walaji wazuri wa chipsi,” amesema na kuongeza kuwa viazi katika soko hilo vinatoka Mikoa ya Mbeya, Njombe, Kilimanjaro na nchini Kenya.

Amesema kwa wastani kwa siku zinaingia gari 20 za viazi za uzito tofauti, hivyo kufanya uwepo wa tani karibu 400 sokoni hapo na kwamba viazi vya Mbeya na Njombe huwa ndiyo tumaini lao kubwa kwa mwaka, huku vile vya Kenya vyenyewe ni kati ya mwezi Julai na Septemba.

” Miezi ya Novemba hadi Mei, viazi vinauzwa kati ya sh 60,000 hadi Sh 100,000 kwa gunia kutokana na hali ya hewa. Lakini kwa sasa gunia moja ni kuanzia Sh 50 000 hadi 55,000,” amesema na kuongeza kuwa soko hilo linahudumia Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Zanzibar.

Masoko mengine yanayouza viazi mkoani Dar es Salaam ni Temeke, Ilala na Mbagala.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *