“Wanafunzi wa kike muwaone kama nyara za serikali”

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewaonya wanaume wanaotamani kuwaoa au kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike wawaone kama nyara za serikali.
“Nawaambia nyie wananchi (vijana wa kiume, wanaume) wawaone nyinyi (wanafunzi wa kike) na atakayetangatanga na nyinyi kuna miaka 30 kuchanganya na umri wako hela.
” amesema.
Abbas ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya wasichana Mtwara Girls iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.
Amesema serikali inafanya kila jitihada kumuwezesha mtoto wa nchini kupata elimu na kufikia lengo lake bila kukatisha masomo.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewata walimu kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu sahihi ili kuwasaidia kufika melengo yao.
Abbas alitembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa majengo ya mabweni pamoja na madarasa na baadae kuzungumza na watoto wa shule hiyo ya wasichana.