‘Wanafunzi wajifunze kwenye maabara mpya’

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa samani, ili kuwezesha wanafunzi wanapoanza muhula mpya wa masomo wajifunze kwenye maabara mpya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).
Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Stanslaus Nyongo wakati ilipotembelea chuo hicho kujionea umaliziaji wa jengo la madarasa, maabara na ofisi za wafanyakazi.
Awali serikali ilitoa Sh bilioni 1.7 kwa lengo la kujenga jengo hilo, ambazo ni fedha za maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko -19.