Wanafunzi wapewa mafunzo afya ya uzazi

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Tabasamu kwa Jamii Nchini (Smile for Community) limetoa mafunzo kuhusu haki ya afya ya uzazi kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Mji Nanyamba Mkoani Mtwara.

Mafunzo hayo yamefanyika wiki hii kwenye Halmashauri hiyo kwa Wanafunzi hao kutoka katika Shule mbili za Sekondari kwenye Halmashauri hiyo ikiwemo Nanyamba, Nyundo na shirikisha Wadau mbalimbali kutoka kwenye Halmashauri hiyo ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na shughuli mbalimbali za Kijamii kwenye Halmashauri hiyo linaloshughulikia masuala ya msaada wa Kisheria Nchini la Pararigo.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Tabasamu kwa Jamii Nchini Flora Njelekela amesema wanapozungumzia masuala ya haki ya afya ni moja kati ya ukatili ambao Mtoto wa Kike amekuwa akipitia hivyo wameona ipo ya kutoa elimu hiyo ili kuleta uelewa kwa Mtoto wa Kike kuhusu haki hiyo.

‘’Wakati tukiwa kwenye kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili wa Wanawake na Watoto, tunawapatia uelewa zaidi Mwanafunzi hasa wa Kike ili waweze kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu haki hiyo kama vile uzazi, hedhi salama, uchumi pamoja na mazingira kwa ujumla lakini pia kumekuwa na ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo suala la Mtoto wa Kike kukosa elimu kwahiyo elimu hii imegusa maeneo mengi ambayo yatasaida kumjenga Mtoto wa Kike kuweza kufikia malengo yake’’,

Amesema kupitia kazi hizo wanazozifanya waligundua kuwa kuna changamoto nyingi ambazo Mtoto wa Kikie amekuwa akizipitia ikiwemo kutembea umbali mrefu kufata elimu hali inayopelekea kupata changamoto tofauti za ukatili wakati akiwa njiani kwa ajili ya kufata huduma hiyo ya elimu.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Mji Nanyamba Thomas Mwailafu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara alisema elimu hiyo ni sehemu chanya ambayo itaenda kukuza ustawi wa Watoto wa Kike na kuzuia vitendo vya unyanyapaa katika afya ya uzazi kwa Vijana na Jamii mzima kwa ujumla hivyo amelipongeza Shirika hilo la Tabasamu kwa Jamii namna ambavyo limekuwa likipambana na utoaji wa elimu hiyo kwenye Halmashauri hiyo jambo ambalo ni kubwa kwao hasa Watoto wao hao wa Kike na wa Kiume.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota ameiomba Jamii kwenye Halmashauri hiyo ‘’Tuwekeze kwenye elimu kwa Watoto wetu ili waweze kupata ujuzi na maarifa yatakayomsaidia kuweza kupambana na maisha yake kwahiyo ndugu zangu lazima tuwekeze kwenya elimu ya Watoto wetu kwani tusipowekeza kwenye elimu tunaiharibu Jamii yetu’’,

Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri hiyo Kamila Mishili ameisisitiza Jamii hiyo kuwa mbabalozi wa kufikisha elimu hiyo katika Jamii iliyopo kwenye maeneo yao kwani kunyamazia ukatili ni ukatili zaidi kwani sasa imefika wakati wa kuvuja ukimya, pale ukatili unapotendeka wachukue hatua ili Mtoto wa Kike apate haki za kufanikisha ndoto zake hivyo elimu hiyo ikawe faida kwa Wanafunzi hao Jamii hiyo kwa ujumla.

Kwa upande wao baadhi ya Wanafunzi hao akiwemo Aisha Hassan kutoka Shule ya Sekondari ya Nanyamba ‘’Nalishukuru sana Shirika hili la Smile for Community pamoja na Viongozi wetu wengine wote waliokuja katika mafunzo haya kikubwa naomba tu huu mradi uweze kuendelea ili sisi wanafunzi tuzidi kunufaika lakini pia elimu hii imenipa uelewa mkubwa sana kuweza kufanya vizuri katika masomo na kufikia malengo au ndoto zetu sisi Watoto wa Kike na kupitia elimu hii tutahudhuria vizuri masomo bila kukosa’’,

Habari Zifananazo

Back to top button