Wanafunzi wote wafike shule Januari 6-8

WAZAZI, walezi wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wote walioandikishwa wawe wameshafika shule ifikapo Januari 6 hadi 8, 2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema ili malengo ya serikali ya kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yaweze kufikiwa ikiwemo sekta ya elimu wazazi na walezi hao wahakikishe wanafunzi hao   wanafika shule ifikapo tarehe hizo.

Hayo yamekuja wakati alipotoa taarifa ya ukamilifu wa shuhguli za ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa shule za awali, msingi na sekondari.

Advertisement

Hata hivyo uandikishaji wa wanafunzi wapya wanaotarajiwa kujiunga na masomo  ifikapo Januari Januari 6 hadi 8, 2024.

Wanafunzi hao wanaotarajiwa kujiunga na masomo katika kipindi hicho wakiwa ni pamoja na darasa la awali, msingi na wale waliyochaguliwa kuingia kidato cha kwanza.

Kwa wanafunzi wa awali matarajio ya mkoa huo yalikuwa ni kupokea wanafunzi 39,758 elfu na waliyoripoti ni 23,114 elfu.

Shule ya msingi makadirio yalikuwa 36,709 elfu ambapo utekelezaji ni 25,739 elfu huku waliyodahiliwa kuingia kidato cha kwanza  ni 28,264 elfu.

Kupitia taarifa yake ya utekelezaji wa miradi iliyowasilishwa leo Disemba 30, 2023 kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) amesema hali ya utekelezaji wa miradi hiyo imefanyika kwa ufanisi mkubwa.

Aidha Mkuu huyo wa meelezea utayari wao wa kuwapokea wanafunzi  hao ifikapo tarehe hizo, “Ukamilifu wa miradi hii unaenda kutoa uhakika wa wanafunzi hao kupata maeneo salama ya kusomea’’amesema Abbas

‘’Nitumie fursa hii kuwashukuru watendaji ,wananchi kwa ujumla na wataalam wote katika utekelezaji wa miradi hii”

Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha ifikapo tarehe hizo wanafunzi wote waliyoandikishwa  wawe wameshafika shule ili malengo ya serikali ya kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi hiyo yaweze kufikiwa.